0


Ninae mchungaji anaenilea kiroho Rev. Mnyamlapi, yeye amewahi kunipa ‘guiding principle’ unapofika muda wa kuchumbia na kuoa. Alisema, “Kadiri unavyozidi kusoma na unavyozidi kufanikiwa kiuchumi na kimaisha ndivyo ugumu wa kumpata mke mwema unavyozidi kuongezeka. Hii ni kwa sababu unapomchumbia binti hutaelewa ikiwa amekupenda wewe ama amevutiwa na mafanikio yako” Pastor akazidi kufafanua, “Mwanaume una mambo mawili:



 1)Jinsia ya kiume: yaani vile ulivyo kimaumbile na kiasili na
 2) Uanaume: yaani yale mafanikio unayokuwa nayo kama mwanaume ikiwemo mali, fedha, elimu, kujiamini, fikra za kiuongozi n.k”. Pastor wangu akendelea, 

“Mwanamke ameagizwa mambo mawili:

 1) Kumtii mume 
2) Kumsaidia mume.

 Ili mke amtii mumewe ni lazima awe anampenda kwa jinsi alivyo yaani kimaumbile na kiasili; lakini mke anaweza kumsaidia mwanaume hata kama hajampenda kwa sababu usaidizi unaotajwa ni kwenye ule upande wa uanaume!” Pastor akanileta kwenye point, “Kibiblia binti ambaye ndiye mke uliyeumbiwa na Mungu anatakiwa akupende wewe kwa jinsia yako (pasipo kuambatanisha na kitu chochote) ambalo hili tunaliita ‘Spiritual Configuration’; lakini kwa asili na saikolojia ya kibinadamu(kimwili) kitu cha kwanza ambacho mwanamke anavutiwa nacho kwako ni uanaume wako. Kadiri unavyokuwa na “uanaume mwingi” ndivyo wanawake wengi wanavyovyutiwa na wewe na kuwa tayari kukusaidia kuyatumia mafanikio yako! Mwisho akanishauri, “Kusoma miaka mingi na kutafuta maisha kunawafanya vijana wengi mshindwe kuoa mapema na mnapotaka kuoa mnajikuta mnapata wanawake ambao wameolewa kufuata mafaniko yenu na sio kuwafuata ninyi. Uwe makini sana kwani ni rahisi mno kuoa mke “mzigo”; ng’ang’ana na Mungu akakuibulie mke mwema na halisi”. Mchungaji akaishia hapo. 


Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top