
~Siri kubwa ya pesa duniani ni kutengeneza THAMANI katika jamiii inayokuzunguka~~
Watu wengi vipato vyetu ni vidogo hii ni kutokana na thamani yetu katika jamii. Usishangae leo hii ndugu yako anaingiza milion moja kwa saa hii ni kwa sababu ana THAMANI KUBWA KATIKA JAMII INAYOMZUNGUKA. Leo hii ewe rafiki yangu jiulize unaingiza shilingi ngapi kwa saa moja. Chukua mshahara wako gawanya kwa week nne then ile pesa ya week moja gawanya tena kwa siku tano. Pesa ya kila siku gawanya kwa masaa. Unalipwa hio pesa ya aibu hii ni kutokana na kukosa THAMANI KATIKA JAMII YAKO. Ndugu yangu jiulize leo mbona una thamani ndogo katika jamii na ndicho kikwazo kikubwa cha mafanikio yako. Kuanzia leo jifunze namna gani ya kutengeneza THAMANI YAKO KATIKA JAMII.
NJIA ZA KUKUZA THAMANI YAKO KATIKA JAMII NA KUONGEZA KIPATO CHAKO
1. Jifunze kutokana na uzoefu wako wa nyuma.
~Jiulize hivi kwa nini ulishindwa kujitatua kiuchumi kipindi hicho cha nyuma na pia panga mikakati namna gani unaweza kujikwamua kiuchumi kwani kama hukufanikiwa itakuwa ndio chanzo cha ubunifu wa mafanikio. Watu wengi hatufanyi hivi ndio mana tumekuwa tukirusha lawama kwa watu wenye mafanikio.
2. Jifunze kutokana na maisha ya watu wengine.
~Kuna namna kuu mbili hapa
kwanza unaweza kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa kwani watakuambia mbinu nyingi walizo tumia mpaka kufikia hatua hizo. Wengi wetu hatupendi kujifunza kwani tunapenda kulisha maneno ya kejeli na lawama kwa watu waliofanikiwa. Lakini mungu ni mkuu kwani nguvu yake haiwezi kupingwa na binadamu tu. Hivyo unapokutana na vikwazo kutoka kwa watu wenye mtazamo hasi usikate tamaa jua mungu anakupigania ipo siku THAMANI YAKO ITAONEKANA.
PILI, Tunajifunza kutoka kwa watu walio anguka kibiashara kwani ndio watu pekee watakueleza udhaifu waliofanya ndipo utakuwa tayar kuweka mikakati dhidi ya madhaifu hayo. Leo hii mtanzania hapendi kusalimiana na mtu mwenye maisha magumu hajui kuwa mtu km huyu ndio nguzo kubwa ya mafanikio kwake tujifunze hayo.
Leo hii namtumia msanii mdogo na mchanga ktk mziki lakini leo hii amekuza THAMANI YAKE KATIKA JAMII. Unaweza ukajionea wewe mwenyewe. Hii ndio siri kubwa ya kuwa na thamani kubwa. Jiulize ni watu wangapi wanasema diamond ni mwizi wa nyimbo? Mara ngapi watu wasiopenda mafanikio hawampendi diamond? Mimi sio mpenzi wa mziki lakini maisha ya kifahari ya DIAMOND, dada yangu Lady jay dee ni kutokana na kuwa na THAMANI KUBWA KATIKA JAMII. Sitakusahau ndg yangu MILLAD AYO kijana unaelipwa pesa ndefu kwani una THAMANI KUBWA KWA JAMII.
Ndg yangu THAMANI ndio kipimo cha kipato chako sio MUDA unaotumia kuitafuta pesa. Thamani hii haitafutwi darasani inatafutwa na kujifunza katika jamii inayotunzunguka. Jifunze kwa hili na badilika.
SIRI YA MAFANIKIO
1. UWE NA NDOTO NA MALENGO
2. JIAMINI KUWA UNAWEZA
3. USIOGOPE VIKWAZO
4. ACHA KUSIKILIZA WATU YENYE MTAZAMO HASI
5.FANYA KAZI KWA BIDII
~~UKIFANYA HAYO NINA IMANI IPO SIKU UTAJIRI WAKO NA THAMANI YAKO ITAKUA NI KITEGA UCHUMU NA UTALII MKUBWA NCHINI TANZANIA NA AMINI IPO SIKU UTAITWA IKULU ILI WAKUONE.
KUMBUKA:SIRI PEKEE YA KUKUZA THAMANI YAKO NI KUJIAJIRI
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.