0


Ukipata nafasi ya kusoma na kuajiriwa, jamii zetu nyingi za Kiafrika zinakuwa na matazamio makubwa kuliko uwezo wako halisi. Kama unatokea kwenye familia zetu za kawaida(za hali ya mtu); wakisikia upo kazini na unalipwa tsh laki tano basi wanaona unapata mahela mengi sana.

 Baba na mama wanataka uwajengee, wadogo zako wanataka uwasomeshe, ndugu wanataka uwe unawakumbuka kwa vi-MPESA, wanataka uhudhurie ama utume pesa katika misiba na sherehe zote za huko kwenu, hapo sijataja wale waliofeli shule nao wanatumwa kwako uone utawasaidiaje! Hayo tisa, kumi ni kwamba hao hao wanaokurundikia majukumu wanataka kuona unapata maendeleo; uwe na gari, nyumba, n.k. 

Ukikwama utaanza kumiminiwa lawama na majungu, ohoo, ajira anayo lakini maendeleo hana! Mara ohoo, tangu apate kazi amewasahau kabisa hasaidii ndugu zake na mengine mengi! Masikini ya Mungu kumbe hawajui kuwa katika hako ka laki tano; laki nzima unalipa pango, laki mbili na ushee inakatika kwenye misosi, laki nyingine nauli na viimejensi kwenda na kurudi kazini;
 Mawasiliano na mavazi vinahitaji pesa, na hapo bado michango ya harusi na sendoff za wafanyakazi wenzio na za marafiki zako ambao huwezi kujikausha eti usichangie; na hiyo michango siku hizi viwango vyake ni maelfu! Hapo bado watoto wako hawajawa wakubwa waanze kusoma kwenye shule za fasheni za akademia! Piga hesabu mwenyewe ni shilingi ngapi inabaki kila mwezi hadi umudu kusaidia kila mtu na hapo hapo unahitaji maendeleo yako binafsi? Si unaweza kufa masikini pamoja na kuwa una ajira? Kimsingi ni kwamba ukipata fursa ya kuajiriwa jitahidi juu chini uanzishe miradi, biashara ama vitega uchumi vya kukuongezea kipato[ili kwamba angalau umudu kuwasaidia wale wa karibu kama wazazi na wadogo zako,]. Lakini ukisema uishi kwa kutegemea mshahara pekee, utaishi kwa shida sana na utabebeshwa hata lawama zisizo na msingi. Tumia mshahara wako kama mbegu!

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top